Tatizo kuu la kisasi cha Sasa.

Kwenye jamii ya kisasa, ubinafsi ni tatizo mkubwa sana,kila mtu anapambana na mambo yake kwa namna yake mwenyewe.

Jamii ya asili walikuwa na ushirikiano mkubwa kuliko jamii ya kisasa.

Hali hii ya ubinafsi imepelekea matabaka kujengeka baina ya watu kwenye jamii .

Tabaka kati ya masikini na tajiri ni kubwa na linazidi kuwa kubwa .

Hali hii inatengeneza upweke ambao umechochea msongo wa mawazo na magonjwa ya akili .

Watu wengi hawana furaha wala utulivu wa akili na mwili licha ya maendeleo makubwa ambayo yametokeo na yanayoendelea kutokea .

Tangu enzi na enzi , ushirikiano mkubwa ulikuwa kwenye vitu viwili,chakula na usalama.

Watu walikuwa tayari kushirikiana kwenye kugawa vyakula Ili kuhakikisha wote wanakuwa na afya njema.

Kila mmoja alishiriki katika kuhakikisha makazi yao ni salama kwa wote.

Sasa maendeleo ambayo yametokeo yameondoa hatari hizo mbili na hivyo mtu anaweza kujitegemea kuanzia chakula hadi usalama.

Hilo limejenga ubinafsi mkubwa ambalo linaendelea kuwa na madhara kwa jamii ,kwa ujumla.

Vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma ni matokeo ya ubinafsi ambao umejengeka kwenye jamii.

Mtu anajiangalia yeye mwenyewe tu na haangalii wengine.

Hatua ya kuchukua,tunahitaji kujenga upya jamii zetu kwa namna ambayo ushirikiano na uwajibikaji unakuwa mkubwa.

Jamii zinapaswa kujengwa kwa kuanzia ngazi ndogo ndogo ambapo watu wanajuana mmoja mmoja.

Kujuana kunaongeza ushirikiano na kutegemeana kunaleta uwajibikaji kwa sababu kila mtu anategemewa kutekeleza wajibu fulani.

Upweke,msongo , ubadhilifu,uuaji na ukuaji wa matabaka ,ni sehemu ya madhara ya jamii ya kisasa.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei

kemeimaureen7@uamsho

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *