Jinsi ya kujitenganisha na dunia.

Tunaishi kwenye dunia ya sasa ambayo tuna muunganiko wa masaa 24 kwa siku 7 za wiki,Ili kuweza kufanya makubwa unahitaji muda wa kujitenganisha.

Watu wote ambao wameweza kufanya makubwa kwenye maisha yao ;waliweza kuwa na muda ambayo walijitenganisha kabisa.

Katika muda huo hawakuwa na internet, Tv ,simu, redio au watu. Walitenga muda wa kuwa peke yao bila ya usumbufu wowote ule kwa muda mrefu.

Na hapo ndipo waliweza kuweka umakini wao kwenye kitu na kuweza kuziona fursa za kipekee ambazo wengine hawazioni.

Ukimya na utulivu ni hitaji kubwa na muhimu sana kwako Ili kuweza kufanya makubwa.

Na katika kipindi hicho ndiyo unaweza kujifunza kwa kina na pia kuzalisha kwa viwango vya juu kabisa.

Ukweli ni kwamba kila mtu anakazana kupata muda au umakini wako ili kukunasa kwenye mambo yake.

Kila biashara inakutaka uwe mlaji wa kile ambacho inauza na siyo tu mlaji,bali ujenge uraibu wa kukigemea.

Kila mtandao wa kijamii na huduma na bidhaa nyingine za kidijitali zinakazana kunasa umakini wako ili uzitumie muda wote.

Huwezi kufanya makubwa kwenye maisha yako kama muda wako umenaswa kwenye vitu mbalimbali.

Unahitaji kipindi ambacho unajinasua kwa kujitengenisha. Unapaswa kutenga muda ambao hakuna kelele au usumbufu wa aina yoyote unaweza kukufikia.

Katika kipindi hicho ni wewe tu na kazi yako, hakuna kingine. Zima simu yako, usiwe kwenye mtandao na mtu yeyote anayeweza kukufikia.

Hiyo ndiyo njia ya kuweza kujitenga. katika zama hizi. Ukiweza kupata siku kadhaa za kufanya hivyo kila mwezi au kila mwaka , itakuwa vyema kama haliwezekani basi pata siku moja ya kufanya hivyo kila siku kwa wiki.

Na kama huwezi kupata siku nzima kwenye wiki,basi chagua masaa ya kufanya hivyo kwa lwa wiki au kwa siku.

Na haijalishi unafanya kozi ya aina gani au unategemewa kiasi gani . Kama ni lazima uwe unapatikana kwa masaa yote 24 ya siku na siku 7za wiki,hutaweza kufanya makubwa.

Huwezi kufanya makubwa kama muda wote umeunganishwa na kukutana na usumbufu ambao wengine nao wanakutana nao pia.

Kuchukua hatua,panga muda wa kujitenganisha wewe mwenyewe Ili uweze kufanya mambo makubwa zaidi.

Mwandishi akupendaye sana.

Maureen Kemei.

http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *