Sisi binadamu huwa tunapenda kuumizana wenyewe,tumeshazoea kuumizwa kiasi kwamba tunawapa watu nafasi mbalimbali za kutuumiza.
Na tunafanya hivyo kwa kuchukuliwa Kila kitu binafsi,kila ambacho mtu anafikiri au kufanya ,tunaona anatulenga sisi,hata kama haina uhusiano na sisi wenyewe.
Njia kuu ambayo watu wamekuwa wanaumizana ni kupitia uongo ,kila unapoenda,kuna watu watakudanganya kwa namna moja au nyingine . Unapokuja kujua ukweli unaumia, kwa sababu unaona walitumia uongo kujinufaisha kwa namna moja kupitia wewe.
Kama unataka kuondokana na maumivu yanayotokana na uongo,tambua kwamba,watu huwa wanadanganya,na hawadanganyi kwa sababu yako,bali kwa sababu zao binafsi.
Usitegemee watu wakuambie wewe ukweli kwa sababu wanajidanganya hata wao wenyewe. Mtu anapokudanganya ,jua tayari amejidanganya yeye mwenyewe. Kwa kujua hili huumii bali unamwonea huruma.
Unapochagua kuwaona watu kama walivyo,bila ya kujichukulia wewe binafsi , huwezi kuumizwa na chochote wanachofikiri,kusema au kufanya. Kwa sababu unajua hawafanyi kwa sababu yao au kwa sababu zao binafsi.
Unachohitaji ili usiumizwe na yeyote yule kwenye maisha ni kujiamini na kujikubali wewe mwenyewe na kisha kuwaona watu kama walivyo na siyo kama unavyotaka uwaone .
Kwa kujua hayo ,utaona jinsi ambavyo kile wengine wanafanya siyo kwa ajili yako,bali kwa ajili yao wenyewe ,hutaumia tena,bali utawaonea huruma.
Kuchukua hatua; unapojijengea tabia ya kuchukulia chochote binafsi unaondokana na changamoto nyingi kwenye maisha. Kama hasira,wivu,huzuni na chuki vyote vinapotea kabisa unapoacha kuchukulia vitu kwa ubinafsi.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
Mwasiliano.
kemeimaureen32@gmail.com.
http://www.uamshobinafsi.com/wp-admin