Umuhimu wa kuchagua fursa moja na kuifanyia kazi.

Rafiki yangu nataka leo tujifunze kutokana na tabia ya punda,punda akiwekewa nyasi upande mmoja na maji wa pili anajikuta njia panda . Anakuwa anataka ale nyasi na pia anywe maji.

Hivyo atabaki hapo akiangalia ni jinsi gani anaweza kupata vyote kwa pamoja. Kinachotokea ni anakufa kwa njaa na kiu wakati amezungukwa na nyasi na maji.

Ambacho punda anashindwa kukijua ni kwamba,japo hawezi kufanya vyote kwa pamoja,anaweza kuanza na kimoja kisha kwenda kwenye kingine. Anaweza akaanza kula nyasi Kisha kwenda kunywa maji.

Rafiki ,kabla hujamshangaa punda kwa kufa njaa huku akiwa na nyasi, hebu rudi kwako, ni fursa ngapi nzuri zimekuzunguka? Na je, katika fursa hizo ni ngapi unazifanyia kazi?

Kwa walio wengi hasa kwenye zama hizi za mafuriko ya fursa, wanajikuta hawafanyi chochote. Wana fursa tano mbele yao na wanataka kuzifanyia kazi zote,kitu ambacho hakiwezekani ,hivyo wanaishia kutofanya chochote .

Suluhisho kwenye hali hiyo ni rahisi,chagua fursa moja na ifanyie kazi mpaka itakapokamilika,kisha nenda kwenye fursa nyingine.

Hata kama una fursa tano mbele yako ,ukiipa kila fursa miaka mitano ya kuifanyia kazi kwa uhakika,utapiga hatua kubwa kuliko kusubiri mpaka uweze kufanyia kazi zote kwa pamoja.

Katika fursa nyingi zinazokuzunguka,chagua moja utakayoifanyia kazi kwa uhakika na kusema hapana kwa nyingine mpaka utakapokamilisha hiyo.

Kisha nenda kwenye fursa nyingine kwa mpango huo huo. Muda utakwenda iwe utachukua hatua au la . Hivyo badala ya kupoteza muda, chukua hatua.

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *