Rafiki yangu mpendwa karibu tujifunze siku ya leo. Wanasema kuwa uaminifu ni sera bora muhimu sana kwenye maisha hasa kazi na kwenye biashara.
Wale wasiowaaminifu wanaweza kufanikiwa kwa muda mfupi,ila hawawezi kudumu kwenye mafanikio hayo kwa muda mrefu.
Kwa kuwa mwaminifu unaweza ukakosa baadhi ya vitu kwa sasa,lakini hilo litakuweka kwenye nafasi ya kupata makubwa mazuri zaidi kwa baadae.
Msingi bora wa kuzingatia maisha na hasa kwenye mauzo ni kujenga uaminifu kwa kufanya kile kilicho sahihi mara zote .
Hata kama unaona mteja hajui,kama wewe unajua basi fanya kilicho sahihi . Kwa sababu kujua kilicho sahihi itakusumbua wewe mwenyewe kwenye nafasi yako na pia itakupotezea wateja.
Kila unapomhudumia mteja wako,jiulize swali hili ‘je,kama mimi ningekuwa ndiyo huyu mteja na nikawa najua yale niliyojua,je ningefurahia kuhudumiwa na mtu wa aina kama yako?’
Kwa kusimamia sera ya uaminifu kwenye mauzo,utaweza kujenga biashara inayokua kwa muda mrefu na yenye manufaa makubwa.
Mteja mmoja amebeba wateja wasiopungua 250. Kama ambavyo sheria ya Girard 250 inavyosema ‘kila mtu ana watu 250 ambao anajuana nao moja kwa moja’. Hivyo jambo unalofanya kwa mtu mmoja,liwe zuri au baya kitafikaia kwa watu wasiopungua 250.
Kama utamfanyia mteja wako kitu kizuri,jua ana nguvu ya kukisambaza kwa watu wengine 250. Na kama utamfanyia mteja wako mabaya,jua atakusema vibaya kwa watu wengine 250.
Kwa kujua sheria hiyo na kuzingatia utaepuka kupoteza wateja ambayo hujakutana nao na pia utakaribisha wateja ambao hujakutana nao .
Kosa kubwa unaloweza kufanya kwenye maisha au kwenye mauzo ni kuona mteja mmoja na usione kama wa umuhimu wowote,labda usimchukulie kwa uzito.
Kwanza mteja hata akiwa peke yake kwa wakati wote ambao anaweza kununua kwenye biashara yako,analeta faida kubwa sana . Kama utamhudumia kwa uaminifu,ataendelea kununua kwako kwa muda mrefu.
Pili ,huyu mteja siyo kisiwa ana watu wake wa karibu. Chochote unachofanya kwa mteja huyo hakiishii kwake tu,bali kunafikia hawa hao wengine.
Hivyo unapomwangalia mteja mmoja,jua kuna wateja wengine wasiopungua 250 walio nyuma yake.
Hatua ya kuchukua; kuwa mwaminifu kwa kila mteja Ili uweze kujenga sifa nzuri itakayosambazwa kwa wateja ambao nao wanakuamini.
Mwandishi wako akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.