Namna ya kupata utulivu wa akili.

Katika zama tunazoishi sasa,ni zama zenye kelele na usumbufu wa kila aina, kupata utulivu wa akili ni kitu kigumu sana .

Hivyo ni kwa sababu kila mtu anawinda umakini wako na kutaka kuteka akili yako.

Kupata utulivu wa akili lazima uzuie kelele na usumbufu visiingie kabisa kwenye akili yako.

Rafiki yangu unaweza kufanya hivyo kwa kuzingatia haya:

1.Usifuatilie habari kwenye TV,redio,magazeti au mtandao.

2. Ondoka kwenye mtandao wa kijamii.

3. Usibishane na mambo ya siasa, mchezo,dini na mapenzi.

4. Usihangaike kufuatilia maisha ya watu maarufu.

Unaweza kujiuliza utajuaje yale yanayoendelea kama hufuatilii habari. Kwanza mengi yanayoendelea kwenye habari kila siku siyo muhimu.

Na yale muhimu kabisa lazima yatakufikia kupitia watu wengine. Njia bora ya kutumia akili yako ni kujifunza kupitia usomaji wa vitabu na makala zenye maarifa yenye tija na unayoweza kutumia kupiga hatua.

Kwani rafiki yangu habari nyingi ni hasi na za kusisimua , unapaswa uachane nayo maana yatakufanya uwe hasi kwenye mambo mengi kimaisha.

Uhasi ukianzia akilini utaathiri mtazamo wako hivyo unajipata umekuwa hasi kwenye kila kitu,hilo linaathiri sana mafanikio yako .

Mwandishi wako akupendaye sana.

Maureen Kemei

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *