Tumeshaona jisni ambavyo hatujifunzi somo sahihi kutoka kwa Warren Buffett kuhusu uwekezaji ambalo ni kuanza mapema na kuacha riba mkusanyiko ifanye maajabu yake.
Kuna mengine ya kujifunza kwake,hasa ambayo hakuyafanya na hivyo kuepuka kupoteza utajiri wake. Tujifunze Ili tujue vitu vya kuepuka kama tunataka kupata na kubaki kwenye utajiri.
Yafuatayo ni mambo mengine muhimu kujifunza kwa Warren Buffett;
- Hajawahi kukopa kupitiliza.
- Hakuwahi kutaharuki na kuuza uwekezaji wake katika midororo ya uchumi 14 ambayo ameipitia katika maisha yake.
- Hajawahi kuharibu jina na sifa yake kwa kufanya mambo yasiyo sahihi.
- Siyo mtu wa kun’gang’ana na njia au mtazamo mmoja.
- Amekua akiwekeza kwa sehemu kubwa fedha zake mwenyewe na siyo kutumia fedha za wengine.
- Hakujichosha na kuamua kustaafu uwekezaji,badala yake amekuwa akienda taratibu bila kuchoka.
- Amevuka magumu na mabaya mengi na kubaki akiwa kwenye utajiri wake, tangu akiwa na miaka 11 mpaka sasa miaka 90 hajawahi kuanguka kwa sababu amekuwa anaepuka yasiyo sahihi.
Kuchukua hatua kupitia haya mambo muhimu ambayo tumejifunza tunapata kujua namna ya kuepuka kupoteza utajiri wetu kwa mambo mbalimbali.
Akupendaye sana.
Maureen Kemei
www.uamshobinafsi.co.ke.