Baada ya kutambua na kujua umuhimu wa kijitambua sisi wenyewe kama binadamu, tunapaswa pia kuzingatia msimamo wetu kwenye maisha .
Kwani kitu kikubwa kinachowazuia watu kuishi maisha halisi kwao ni kukosa msimamo. Wengi huwa wanabadilika badilika kila mara, kiasi kwamba hawawezi kuaminiwa au kutegemewa kwenye kitu chochote.
Wengi ni watu wa kubadili mawazo yao haraka na ndani ya muda mfupi. Wakati huu wanaamua hiki,ila baada ya muda mfupi wanaamua kingine ambacho ni tofauti kabisa na kile cha awali. Kwa kubadilika badilika huko,watu wanashindwa kuwa halisi na hata kutokuaminika.
Wastoa wanashauri mambo mawili muhimu ya kuzingatia Ili kujijengea msimamo:
Jambo la kwanza ni kuwa na maisha ya aina moja,hadharani na faraghani. Watu wengi huwa na maisha ya aina mbili,mbele ya watu wanajionyesha ni watu wa aina fulani, ila wakiwa sirini wanakuwa ni watu wa aina tofauti.
Wewe chagua kuwa mtu wa aina moja,mwenye maisha ya aina moja, hadharani na sirini . Kusiwe na chochote unachokificha kwenye maisha yako. Ukishakuwa na maisha ya aina mbili, huwezi kuishi kwa uhalisia wako na unakosa msimamo wa ndani.
Jambo la pili ni kuchagua aina ya mtu unayetaka kuwa na kuwa huyo mara zote. Ukishachagua unakuwa mtu wa aina gani,basi kuwa hivyo bila kubadilika.
Haimaanishi hubadili unayofanya kulingana na mabadiliko yanayotokea, bali inamaanisha kuwa mtu wa aina moja mara zote .
Kuchukua hatua; rafiki yangu maisha yasiyo na msimamo ni maisha yasiyoeleweka . Chukua hatua ya kujijengea msimamo kwenye maisha yako kwa kuamua unakuwa mtu wa aina gani na kisha kuchagua kuwa na maisha ya aina moja .
Akupendaye sana.
Mwandishi Maureen Kemei,
Mawasiliano:
kemeimaureen7@gmail.com.
www.uamshobinasfi.com.