Pata picha rafiki yangu unafanya kazi na wenzako ofisini lakini wanapenda sana kushusha. Ukikosea kidogo wanakusema vibaya kwa bosi yako,hivi utajiskiaje kama watakuwa wanakusema vibaya kila mara na unajua kabisa wanasema uongo juu yako.
Bila shaka utajiskia vibaya tena sana na kutamani kubadilisha kazi au kuacha kazi hiyo. Au labda utatamani kujaribu kuwafurahisha wenzako maana unaamini kwa kuwafanya wengine wafurahi ndio watakupenda zaidi.
Kabla hujafanya mà amuzi ya kubadili ofisi unaofanya kazi najua utajaribu kutumia nguvu na akili zako kuwafanya waache tabia hiyo. Maana tayari unajua kwamba kufanya mema ndio njia ya kupata umakini wa wengine.
Najua nyuma ya akili yako ungetamani wangeacha tabia zao za kukusema vibaya na kukutafutia makosa hata ambayo hujayafanya. Sina uhakika kama itakufaa, lakini labda wewe ni mtu ambaye hutaki mzozo,unajiambia kama ungeweza kuwafanya wenzako waache tabia hiyo ya kuleta mzozo na vurugu( kila kitu kingekuwa sawa kwa uhakika kabisa).
Anayependa kufurahisha watu kwa mfano akiona gari likija kwa mwendo wa kasi,anamwondokea au anaendesha gari yake kwa kasi zaidi ili amwondokee,kwa sababu anafikiri mwenzake ana araka zaidi na hataki kumkasirisha kwa kuendesha polepole.
Wanaofurahisha watu wanaogopa sana kukataliwa au kuachwa,hiyo ndio hofu kubwa ambalo wanaiogopa sana. Akili yao wana mentality ya ” kama sitakufanya ufurahi,basi hutanipenda.”
Kitu kimoja zaidi kwa wanaopenda kufurahisha wengine ni kwamba wanastawi kwa kusifiwa na kupewa uhakikisho kutoka kwa wengine, na kama hawapokei sifa hizi za kuimarishwa vya kutosha, wanabadili tabia zao na kujaribu wawezalo kuwafanya watu wafurahi .
Kuchukua hatua, rafiki yangu tabia ya kutaka kufurahisha kila mtu inachosha kwa kweli. Ni vizuri kufuata sauti yako ya ndani na kukataa kufuata watu wanasema juu yako. Maana kwa kusikia sana sauti za nje utaumia mwenyewe kwa kutafuta sababu za kuwafurahisha wengine ilhali wewe unaumia .
Akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
http://www.uamshobinafsi.com