Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Ili kujijengea umakini mkubwa kwa kitu chochote unachofanya, unapaswa kuweka fikra zako zote kwenye kitu hicho.
Kwa kawaida fikra zetu huwa zinazurura hazikai eneo moja kwa muda mrefu. Lakini fikra hizo zinaweza kudhibitiwa na kuwa vile mtu unavyotaka.
Katika kuzidhibiti fikra hizo,tambua pale zinapotoka kwenye kile unachofanya na kwenda kwenye kitu kingine kisha zirudishe kwenye kile unachofanya.
Kuwa mlinzi wa fikra zako mwenyewe, hakikisha zinakaa kwenye kile unachofanya badala ya kuzurura kwenye vitu vingine.
Kufanya jambo moja kwa wakati pia inasaidia sana kujenga umakini wako. Wapo wanaodhani kufanya mambo mengi kwa pamoja ni kuongeza ufanisi. Lakini siyo kweli, inashusha umakini na kuathiri ufanisi.
Panga kufanya jambo moja kwa wakati, weka fikra zako zote kwenye jambo hilo unalofanya kwa wakati unapofanya mpaka likamilike au muda uliopanga kulifanya uishe.
Kudhibiti mazingira yako pia ni muhimu kwenye kujijengea umakini. Kama mazingira yana usumbufu mkubwa, umakini wako utasumbuka.
Kuchukua hatua rafiki yangu fanya kitu kwenye mazingira tulivu ambayo hayahangaishi umakini wako ili fikra zako ziweze kutulia kwenye kile unachofanya.
Akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.