Sababu nzuri ya kusema hapana.

Rafiki yangu mpendwa Ili uweze kusema hapana kwenye mambo yasiyo sahihi,lazima uwe na mambo sahihi unayosema ndiyo.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini lazima ndiyo yako iwe kubwa na muhimu kuliko hapana.

Utajisikiajie kama utasema ndiyo kwenye mchakato unayofanyia kazi na sema hapana kwa mengine yote ambayo hayasaidii mchakato huo.

Kitu kimoja zaidi ni kuwa ndiyo hapana zako zitawaumiza watu muda mfupi,lakini zitawasaidia kwa muda mrefu kupitia kile unachofanya, ambayo kwa kusema hapana kwenye mengine utakifanya kwa ubora sana.

Lazima pia uwe na kiasi kwenye hapana zako,maana iwapo utasema hapana kwa kila kitu,itakuwa ni njia nyingine ya kujificha au unaweza kuwapoteza wale muhimu unaowahitaji sana kwenye kile unachofanya.

Pata picha ulisema ndiyo kwenye mambo mengi nako unakosa muda na umakini wa kutosha kwenye kile muhimu unachofanya.

Kuchukua hatua, kwa kuwa tumeona ndiyo yetu lazima iwe kubwa na muhimu kuliko hapana. Hivyo inatupasa tuweke vipaumbele vyetu kwa usahihi,tunasema ndiyo kwa yanayohusiana na vipaumbele vyetu na hapana kwa yasiyohusiana na vile vipaumbele vyetu.

Habari njema rafiki yangu ni kuwa usiogope kuwaumiza watu kwa muda mfupi kwa hapana zako,kwani baadaye watanufaika na matokeo utakayozalisha.

Akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *