Rafiki yangu mpendwa pata picha kuna mtu unamwamini sana na kumtegemea kwa asilimia zote, kiasi kwamba huwezi ukafanya maamuzi bila ruhusa yake.
Utajiskiaje kama mtu uyo anakuhadaa tu mwishowe anakutawala kwa sababu ulimpa nafasi ya kukutawala mwanzoni.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini kutoka kwenye kitabu cha the fountainhead by Ayn Rand, tunaona jinsi riwaya hii inavyotuonesha mwusika Ellisworth M.Toohey. Anaoneshwa kama mtu anayependa kuonekana ni mzuri mbele za watu Ili tu apate nafasi ya kuwatawala na kuwahandaa watu hao.
Toohey alikuwa na sifa ya kuhakikisha watu hawafanyi kile wanachopenda, bali kile ambacho kinawasaidia wengine. Hasa pale anapogundua mtu anakipenda kitu sana,basi alimshauri asikifanyie kazi,hasa wakati wa mtu kuchagua asomee nini. Aliwaepusha sana vijana wasifuate kile wanachopenda, bali wafuate kile ambacho kitawasaidia watu. Aliamini mtu kusomea kile anachokipenda ni ubinafsi, na kusomea kile chenye manufaa kwa wengi ndiyo sahihi.
Toohey aliwafanya wafuasi wake wamtegemee yeye,hivyo hawakuweza kufanya maamuzi bila yeye, na pia alikuwa akiwaambia kitu hawapingi,bali wanaiamini na kukifanya.
Toohey aliendelea na falsafa yake ya kuwaweka wengine mbele kuliko maslahi yake mwenyewe. Kwa kufanya hivyo,aliweza kutengeneza wafuasi, ambao walimchukulia Toohey kama mtakatifu, mtu asiye na ubinafsi na kukosea.
Aliamini kwamba ili mtu kufikia wema, mtu unapaswa kuweka maslahi ya wengine mbele kabla ya maslahi yake binafsi. Aliamini mtu hapaswi kujijali yeye mwenyewe kwa namna yoyote ile, bali kujali wengine kwanza. Kwa kifupi falsafa ya Toohey ilikuwa ni ya ujamaa, ambapo kundi ni bora kuliko mtu mmoja mmoja.
Rafiki yangu tunayojifunza kwenye maisha ya Toohey ni kwamba, tunapaswa kuwa makini sana na wale wanaoonekana kuwa wema sana, lakini ndani ni mtu mbaya na mwenye nia ovu.
Kitu kimoja zaidi tunapaswa kuepuka kumwamini mtu yeyote kiasi cha kumtuhusu atufanyie maamuzi muhimu ya maisha yetu. Hicho ni kitu ambacho kila mmoja wetu anapaswa kukifanya wenyewe. Kwa kwa kuwapa wengine ruhusa hiyo tutakuwa tumeruhusu atutawale. Kumbuka kwamba kila mtu ana ajenda zake kwa jambo lolote lile,japo nje ataonekana hana ajenda, lakini zipo.
Kuchukua hatua, kama ambavyo tumejifunza hapa kwamba, tusiwape wengine ruhusa ya kufanya maamuzi kwa ajili yetu, tunapaswa kujiamini na kujisimamia kwenye kufanya maamuzi yetu sisi wenyewe, ili tuwe huru wa kufanya kile tunachokipenda bila kupingwa na yeyote yule.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
.