Mambo 10 ya kubadili leo hili kufikia mafanikio makubwa.

Rafiki yangu mpendwa, kila mtu anataka mabadiliko, anataka maisha yake yawe bora, anataka kuwa na kazi au biashara mzuri, anataka kuwa na familia bora,anataka kuwa na uongozi mzuri na mengine mengi mazuri. Lakini linapokuja swala kwamba inabidi mtu abadilike ndio changamoto inapoanza.

Kila mtu anataka aendelee kufanya kile ambacho amezoea kufanya, anataka kuendelea na maisha ambayo ameyazoea, lakini anataka kuona mabadiliko makubwa. Hii ni ndoto ya mchana ambayo haiwezi kutokea kwa njia yoyote ile.

Rafiki yangu mabadiliko yanaanza na wewe na ndio vitu vingine vinabadilika, unabadilika kwanza wewe na ndio kazi yako, biashara yako,mwenza wako, watoto wako, wafanyakazi wako na jamii inayokuzunguka wanabadilika. Haiendi kinyume na hapo, kwamba hivyo vingine vyote vikishabadilika basi na wewe ndio utabadilika,hakuna kitu kama hicho.

Kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako? Haya ni mabadiliko kumi unayotakiwa kuyafanya sasa, kama imekuwa bado huyafanyi.

Moja ni kuwa na matumizi mazuri ya muda wako,usiupoteze kwa mambo yasiyokuwa na msingi kwako.

Pili ni usishiriki kwenye majungu,umbeya au kumsema mtu yeyote vibaya.

Tatu weka juhudi kubwa sana kwenye kazi yako,nenda hatua ya ziada, fanya zaidi ya mtu mwingine yeyote.

Nne acha matumizi mabovu ya fedha,nunua vitu ambavyo ni muhimu kwako.

Tano acha kukaa na watu ambao wanakurudisha nyuma.

Sita pata muda wa kukaa na familia yako na wale unaowapenda.

Sapa usinunue kitu ili kuonekana,au kwenda na wakati.

Nane kuwa mwaminifu,kuwa mwadilifu.

Tisa timiza neno unaloahidi

Kumi sema hapana mara nyingi uwezavyo jambo lolote ambalo halina manufaa kwako au halitakufikisha kwenye malengo yako sema hapana

Kuchukua hatua,unajua hakuna mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kutokea nje yako. Mabadiliko yoyote ya kweli yanaanza ndani yako mwenyewe rafiki yangu. Tunapaswa kuamua na kuchukua hatua ya kufanya mabadiliko kwenye maisha yako na wengine wanaokuzunguka bila shaka nao watabadilika.

Akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@kemeimaureen

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *