Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna hofu ya nje na ya ndani. Tumelelewa tangu utotoni na woga mwingi si kwa nje tu,bali pia kwa ndani.
Hofu ya nje ni kama vile kupoteza kazi, kutokuwa na chakula cha kutosha, kupoteza nafasi yako, bosi wako kuwa na tabia inayo kuumiza.
Hofu ya ndani ni kama hofu ya kutokuwa, hofu ya kutofanikiwa,hofu ya kifo,hofu ya upweke,hofu ya kutopendwa na hofu ya kuchoka kabisa.
Chanzo kikubwa cha hofu ni utegemezi wa vitu,watu au mawazo huzaa hofu, utegemezi unatokana na ujinga,kutokana na ukosefu wa kujitambua, hutokana na umaskini wa ndani yaani wa fikra, hofu husababishwa kutokuwa na uhakika kiakili, huzuia mawasiliano na uelewa.
Kupitia kujitambua tunaanza kugundua na hivyo kuelewa sababu ya hofu, sio tu ya juu juu lakini sababu kuu za hofu kwa ujumla.
Hofu inapatikana au inatafutwa, inahusiana na wakati uliopita, na kwa hisia huru ya mawazo kutoka kwayo, wakati uliopita lazima utazamwe kwa jicho la sasa.
Mambo yaliyopita yanataka kuzaa mambo ya sasa ambayo inakuwa kumbukumbu ya kutambua ubinafsi wako yaani ‘mimi’ na ‘vyangu’ . Ubinafsi ndio mzizi wa hofu yote.
Kuchukua hatua, Ili kuondokana na hofu ya mambo yaliyopita ni bora kujitambua wewe ni nani ili litakusaidia kuepukana na mawazo yanayochangia hofu kwenye maisha yetu.
Akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.