Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna sababu kubwa mbili za watu kushindwa kufanikiwa kwenye mambo yao wanayoyapanga.
Mosi, Ni kukosa Nidhamu (Indiscipline)
Nidhamu ni uwezo wa kufanya jambo unalotakiwa kufanya bila kujali kama unajisikia kufanya au laa,
Ni uwezo wa kufanya jambo muhimu bila usimamizi wala kuhimizwa na mtu yeyote yule.
Ni hali ya kuwa na nguvu ya kila wakati kufanya jambo lako muhimu bila kutoa visingizio.
Kwenye maisha lazima ujiwekee nidhamu na uhakikishe unasimamia nidhamu hiyo; Kwa mfano nidhamu ya kusoma vitabu, nidhamu ya fedha, nidhamu ya kuamka mapema, nidhamu ya kutumia muda wa vizuri bila kupoteza nk
Mbili, Kukosa nguvu ya mwendelezo (Inconsistance)
Kufanya jambo kwa mwendelezo ni nguzo muhimu sana kwenye mafanikio yoyote.
Hakuna namna unaweza kufanya jambo mara moja na kisha ukapata mafanikio mara hiyo moja.
Mara nyingi, utahitaji kufanya jambo mara nyingi, utahitaji mfululizo wa kutenda. Utafanya utakwama na utapambana hadi mwisho utafaninikwa kukamilisha jambo hilo.
Kuchukua hatua kwa ujumla rafiki yangu, bila mwendelezo wa kufanya jambo bila kuacha hakuna mafanikio. Na pia bila kuweka nidhamu kali ya kuamua na kufanya hakuna mafanikio.
Akupendaye sana.
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.