Sifa zinazowatofautisha wanaofanikiwa na wanaofeli.

Rafiki yangu mpendwa kuna msemo unasema, there is nothing useless as doing efficiently that should not be done at all. Ikimaanisha kuwa hakuna kitu kisicho na maana kama kufanya kwa ufanisi jambo ambalo hukutakiwa kufanya kabisa.

Ni kama kuandika majibu ya swali yasiyo yenyewe (O.P) – (Off Point).

Wanaofanikiwa na wanaofeli hutofautiana kwenye kufanya au kutokufanya mambo haya mawili

Mosi, Mambo mepesi na yasiyo muhimu.

Hapa ndio watu wengi hutumia siku yao kwa masaa mengi. Watu wasiofanikiwa hupenda kufanya vitu vyepesi visivyo na umuhimu kama vile kutembelea mitandao ya kijamii, kupiga story na kadhalika wakati ana kazi ngumu   na za muhimu zinazotakiwa kufanyika lakini hazifanyi. Hivi ni vitu ambavyo haviongezi chochote kwenye mafanikio ya mtu, badala yake vinamkwamisha pasipo yeye kujijua.

Mbili, Mambo magumu na ya muhimu.

Haya ndio mambo yatakayokutofautisha na wengine kwa haraka, ni mambo yanayoleta mafanikio.

Ni mambo kama kusoma vitabu, kujiendeleza kimaarifa, kuweka akiba, kuwekeza nk. Wana michezo wanatumia kanuni hii kufanya mazoezi mazito wanayowaongezea uwezo wakati wengine wamepumzika..
 

Epuka mambo madogo madogo yanayokupotezea mwelekeo

Kama unajua ni wapi unaelekea kimalengo ni lazima kila siku kujikagua na kuhakikisha upo kwenye uelekeo sahihi wa malengo yako.

Epuka kabisa kwenda nje ya malengo yako hata kama ni kwa sekunde moja, kwa sababu mtu anayepotea kwa maili 1,500 huanza kupotea kwa sekunde.

Hivyo hakikisha unajikagua mwelekeo wako kila mara.

Mambo ambayo hutakiwi kuyavumilia kabisa ili usipoteze mwelekeo ni pamoja na haya yafuatayo:-

Mosi, Kutojiingiza kwenye majukumu yasiyo ya lazima.

Tunaishi katika ulimwengu wa social network (mitandao ya kijamii). Usipokuwa makini utajikuta kila mara unafanya vitu ambayo havina umuhimu kama kufuatilia habari, kuwafuatilia watu nk.

Vitu hivyo haviongezi chochote kwenye mipango na malengo yako.

Mbili, Kagua mtandao wa mahusiano yako.
Watu unaohusiana nao kwa karibu wana nafasi kubwa ya kukuathiri, kukurudisha nyuma au kukusogeza mbele kimalengo.

Ushawishi mdogo mdogo wanaotupatia unatosha kukuondoa kwenye misingi na njia ya mafanikio.

Tatu, tambua tabia zinazoweza kupoteza mwelekeo wako.

Kuna baadhi ya tabia kama unazo hata kama ungelikuwa mtu bora kiasi gani, anguko lako linakuwa lipo jirani.

Tabia hizo ni kama vile, kupenda sana usingizi kuliko kawaida, uvivu wa kusoma, kushindwa kutunza ahadi zako, kutokuweka akiba, kutozingatia bajeti yako, kutokutunza siri, ulevi  na kutokupenda kazi.

Kuchukua hatua ni wakati sasa rafiki yangu wa kuepuka tabia ambazo zinatuangusha na kujenga tabia zinazovuta mafanikio kwenye maisha yetu.

Akupendaye sana.

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *