Jinsi hofu ya kupitwa inavyokutesa.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini katika ulimwengu wa sasa ambao zaidi ya asilimia 99, ya watu hulala na simu zao kitandani.

Lakini pia takwimu zinaonesha kuwa asilimia 80 ya watu hushika kwanza simu zao na kuangalia habari, na taarifa mbali mbali kabla ya kuamka na kutoka kitandani.

Simu ndiyo inakuwa kitu cha mwisho kushika wakati analala na cha kwanza kushika pale anapoamka . Imekuwa ni kama sehemu ya kiungo cha mwili wa mwanadamu.

Si hivyo tu, mtu yuko tayari kushika simu na kujua yanayoendelea mtandaoni na ulimwenguni, lakini hajui hata kama mguu wake ni mzima.

Achilia mbali kama amelala na mwenza wake ndio kabisa, ataanza kujua yanayoendelea huko kitandani kabla ya kujua hali ya mwenza wake huyo aliyenaye karibu.

Hali hii inatokana na hofu ya kupitwa na yale yanayoendelea mtandaoni. Hutaki kupitwa unataka uwe wa kwanza kujua kila kitu kinachoendelea ulimwenguni.

Mitandao ya kijamii na hata vyombo vya habari wanajua siri hii. Unahofu ya kupitwa na habari, na matukio mbali mbali yanayokuwa yakiendelea mtandaoni . Ukipitwa unajiskia vibaya. Na hivyo wanatumia mtego huo kukunasa.

Ili uweze kujinasua katika mtego huu unapaswa, kuitawala hofu yako ya kupitwa na yale yanayoendelea mtandaoni. Uitawale hofu yako kwa sababu, usipofanya hivyo wenyewe mtandao na vyombo vya habari wanaitumia hofu yako hiyo kwa faida yao wenyewe.

Siyo kila taarifa au habari zinakufaa wewe kuzijua. Kama habari au taarifa haikuongezei maarifa au fundisho, jua kuwa haikufai.

Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kama vile runinga, redio na magazeti, vinawinda umakini wako. Umakini wako ilipotea, muda na nguvu zako pia zinapotea, hivyo hutaweza kutimiza malengo na maono uliyonayo.

Kuchukua hatua rafiki yangu, tunapaswa kuitawala hofu ya kupitwa ili tusipoteze nguvu na muda wetu kwenye mtandao na habari mpasuko, kwani hatutaweza kutimiza malengo yetu.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei .

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *