Njia mbili za kuishi maisha yako hapa duniani.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuna njia kuu mbili za kuishi maisha yako hapa duniani.

Njia ya kwanza ni kuishi kama ambavyo watu wanataka wewe uishi, Ufanye yale ambayo watu wanakutegemea uyafanye hata kama sio yanayokufurahisha au sio muhimu kwako.

Ufanye kile ambacho kila mtu anafanya hata kama huna msukumo wowote wa kufanya hivyo, hii ndio njia ya kwanza ambayo asilimia 99 ya watu kwenye jamii yoyote wanaishi njia hii.

Njia ya pili ni kuishi kama vile ambavyo wewe mwenyewe unataka kuishi kufanya kile ambacho ni muhimu kwako na una msukumo wa ndani wa kukifanya.

Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuweza kufikia ndoto zako kubwa, bila ya kujali wengine wanafanya nini au wanasema nini.

Kutokujiwekea ukomo wapi unapoweza kufika na kuwajali wale wanaokujali, hii ni njia ya pili ambayo asilimia 1 ya watu kwenye jamii yoyote wanaishi njia hii.

Rafiki yangu, umechagua kuishi njia ipi? Huu ni uchaguzi wako, kama hujachagua au hujui uchaguzi wako ni sahihi au la.

Lakini nikukumbushe kwamba hii ni asilimia 1 wanaoishi maisha kwa njia ya pili, ndio wanaofika mafanikio makubwa sana wanaokuwa na furaha kwenye maisha yao na ambao hawana majuto kwenye maisha yao.

Hatua ya kuchukua; rafiki yangu habari njema ni kwamba maisha ni kuchagua, na kuna njia mbili za kuweza kuishi yako, naamini upo kama mimi unachagua njia ya kuishi asilimia 1 ambayo utafanya mambo muhimu kwako ili uhakikisha maisha yako yanakwenda vile unavyopanga.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *