Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini amani na furaha ni ujuzi ambao kila mtu anaweza kujifunza na kujijengea.
Siyo vitu ambavyo mtu anazaliwa navyo au kurithishwa na wala havitokei kwa bahati mbaya, vinatengenezwa.
Kila mtu anaweza kujijengea amani na furaha na kukuza viwango vyake kama anaamini inawezekana na kujua hatua sahihi za kuchukua Ili kufikia hilo.
Kama ilivyo kwenye kazi, mahusiano, biashara na fedha, furaha pia ni ujuzi mbao mtu anaweza kujijengea anapojua hatua sahihi za kuchukua.
Hatua ya kwanza kwenye kujijengea ujuzi wa amani na furaha ni kukubali na kuamini kwamba vitu hivyo ni ujuzi unaoweza kujijengea.
Hii ni gumu kwa sababu kwa maisha yako yote imekuwa unaamini tofauti na hivyo. Lakini unapoamini na kuchukua hatua, unapata matokeo ya tofauti.
Furaha ni matokeo ya tabia ambazo mtu unakuwa umechagua kuziishi kwenye maisha yako. Wakati unazijenga tabia unaweza usione madhara yake, lakini zinapokuwa zimeimarika ndiyo unaona jinsi zilivyo na madhara kwenye maisha yako kwa ujumla.
Kitu kingine kinachoathiri furaha ya mtu ni mahusiano anayojijengea. Kama mtu anazungukwa na watu wasio na furaha, watu ambao wanafikiri hasi, wamekata tamaa na hawana furaha, ni rahisi kwa watu kubeba tabia hizo kutoka kwa wanaomzunguka. Unapaswa kuwa makini na furaha yako kwa kuhakikisha unaozungukwa nao watu wenye furaha pia.
Kuchukua hatua; tunapaswa kuchagua kwa umakini watu wa kushirikiana nao kwenye mambo mbalimbali. Na muhimu zaidi tuepuke watu wanaopenda ugomvi, maana hao huwa hawakosi kitu cha kugombana.
Pia mtu yeyote unayechagua kufanya naye kazi, hakikisha unamkubali kwamba unaweza kufanya naye kazi kwa maisha yako yote, kama huwezi hivyo, usifanye naye hata kwa siku moja.
Yakubali maisha yako na jihusishe na wale walioyakubali maisha yao na wenye furaha.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.