Namna ya kuchagua kuwa wewe.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini umekuwa unahangaika kujiambia unapaswa kuwa hivi, kufanya kile au kuwa kama wale. Yote hayo huyahitaji.

Unachopaswa kufanya ni kile unachotaka kufanya, kile kinachotoka ndani yako na siyo kuiga wengine. Unapochagua kufanya kile unachotaka, kwa kujisikiliza wewe mwenyewe, unakuwa umechagua kuwa wewe.

Kama unataka kuwa wa tofauti duniani na kuepuka ushindani wa wengine, basi chagua kuwa wewe. Hakuna anayeweza kukushinda wewe kuwa, kwa sababu hakuna aliye kama wewe.

Jifunze kupitia wengine, lakini usijaribu kuiga, usitake kuwa kama mwingine yeyote, jifunze utakavyo, lakini kuwa wewe, ambaye inazidi kuwa bora zaidi kila siku.

Kila mtu kuna kitu cha pekee alichonacho, kuna ujuzi, uwezo na msukumo wa kipekee ulio ndani yako ambavyo kwa wengine hakuna.

Mtu anachagua kuwa yeye na kuuishi utofauti wake, hakuna anayeweza kumshinda, kwa sababu hakuna aliye na vile alivyonavyo yeye.

Lengo lako kwenye maisha ni kutafuta watu ambao wanakuhitaji wewe kweli, wananufaika na kile cha kipekee unachoweza kufanya na Kisha kuwapatia watu hao kitu hicho. Hiyo ndiyo njia ya uhakika kufanikiwa.

Hatua ya kuchukua; baada ya kuchagua kuwa wewe, unapaswa kuwa na hamasa na msukumo mkubwa wa kufanya kile ambacho wewe tu ndiye unayeweza kufanya.

Tunapaswa kuwa tayari kukifanya kwa viwango vya juu na kwa muda mrefu hata kama hakuna anayekulipa.

Ni kiwango hicho cha msukumo ndicho kitazidi kukutofautisha na kuwafanya wengine wawe tayari kukulipa kwa manufaa unayowapa.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *