Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini vile ulivyo ni matokeo ya mtazamo ambao unao.
Matokeo unayoyapata yanatokana na mtazamo wako. Huioni dunia na mambo kama yalivyo, bali unaona kama ulivyo wewe. Hivyo ili kuona vitu kwa namna ambayo itachangia wewe ufanikiwe, unapaswa kubadili mtazamo ulionao.
Kuna nyenzo tano muhimu za kufanyia kazi ili uweze kubadili mtazamo wako.
Ya kwanza ni fikra unazokuwa nazo, unapaswa kuwa na fikra chanya na za uwezekano badala ya fikra ya hasi na za kushindwa.
Ya pili ni hisia zinazokutawala, unapaswa kuwa na hisia chanya juu ya mambo, hisia zinazokusukuma kuchukua hatua sahihi.
Ya tatu ni maneno unayotumia, unapaswa kutumia maneno chanya na ya kuinua na siyo maneno hasi na ya kuangusha.
Ya nne ni matendo unayofanya, yanapswa kuwa matendo sahihi kwako kukupa matokeo unayotaka.
Ya tano ni ushawishi unaokuzunguka, unapaswa kuzungukwa na ushawishi chanya, unaokusukuma kuwa bora na siyo hasi unaokukatisha tamaa.
Kuchukua hatua; rafiki yangu tukifanyia kazi nyenzo hizi tano, tutabadili kabisa mtazamo wako, tutaiona dunia na mambo yanayokutokea kwa namna bora na kuweza kutumia kufanya makubwa zaidi.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.