Umuhimu wa kuwa mnyenyekevu.

Rafiki yangu mpendwa Robin kwenye kitabu chake cha ‘everyday manifesto’ anatushirikisha hadithi ya kipindi akiwa mtoto, familia yao walikuwa mapumzikoni.

Siku moja wakiwa kwenye gari njiani wakapishana na gari la aliyekuwa mpiganaji maarufu Muhammad Ali.

Mama yake Robin alimtaka baba yao aliyekuwa anaendesha gari ageuze na kuifuata gari ya Muhammad Ali.

Walifanya hivyo mpaka kuikaribia na akaanza kumsalimia kwa mbali na kumwomba wapige picha ya pamoja.

Robin na kaka yake waliona ni kitendo cha aibu kwani mtu maarufu kiasi kile asingekubali kupiga picha na watu wasiojulikana.

Lakini cha kushangaza Muhammad Ali alipaki gari pembeni, akawasalimia vizuri kisha akapiga nao picha.

Robin anasema hakuwahi kusahau tukio hilo kwa maisha yao yote. Moja ya picha yao na Muhammad Ali iliwekwa kwenye saa ya ukutani na kuwa inakaa sebuleni kwao.

Kitendo hicho cha unyenyekevu mkubwa walioonyeshwa na mtu aliyekuwa na umaarufu mkubwa kilimpa funzo kubwa Robin.

Hapa tunajifunza umuhimu wa kuendelea kuwa wanyenyekevu hata baada ya kufanikiwa sana.

Kuchukua hatua; rafiki yangu kuna kitu kidogo sana unaweza Kufanya, ambacho hakikugharimu chochote, lakini likawa ni alama kubwa sana kwa wengine.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *