Hatua 3 za kuvunja imani zenye ukomo.

Rafiki yangu mpendwa ili uweze kuwa huru kufikiri na kufanya makubwa, lazima kwanza uvunje imani zote zenye ukomo ulizonazo.

Hapa kuna hatua tatu za kuvunja imani hizo.

Hatua ya kwanza ni kutambua imani za ukomo ulizonazo. Jisikilize sauti zinazotoka ndani yako, kwenye kila unachojiambia huwezi au haiwezekani, jua hapo una ukomo wa kiimani.

Hata kama ni jambo dogo kiasi gani, kama unajiambia huwezi au haiwezekani, jua hapo una ukomo wa kiimani.

Hatua ya pili ni kuangalia ukweli. Mengi unayojiambia huwezi au haiwezekani siyo kweli, ni mazoea tu umekuwa nayo.

Chukua hatua ya kuangalia ukweli kwenye kila eneo ulilojiwekea ukomo. Utagundua kuna wakati uliweza kufanya yale uliyojiambia huwezi.

Na hata kama ulifanya na ukashindwa, matokeo hayakuwa mabaya kama ulivyotegemea yawe. Kwa kuona ukweli huo, utazidi kuona jinsi imani uliyonayo siyo sahihi.

Hatua ya tatu ni kutengeneza imani mpya isiyo na ukomo kwenye maeneo yote ambayo umejiwekea ukomo. Kila unachojiambia huwezi au haiwezekani, jiambie unaweza na inawezekana.

Kwa kubadili imani yako kwenye maeneo uliyokuwa na ukomo, unaacha kuona ukomo na kuanza kuziona fursa mbalimbali za uwezekano.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *