Rafiki yangu mpendwa mwandishi Robin anatushirikisha hadithi ya mwanamuziki Gord Downie, ambaye alikuwa mwimbaji wa bendi maarufu nchini Canada.
Alikuwa anajituma sana kwenye muziki wake na kupendwa na wengi. Siku moja akaanguka na kupata degedege kali.
Baada ya vipimo aligundulika kuwa na uvimbe kwenye ubongo. Uvimbe ambao hauwezi kupona na maisha yake hayakuwa marefu.
Alishauriwa aache shughuli zote nzito na apumzike. Lakini Gord hakukubali, aliandaa ziara ya mwisho na bendi yake ya kuzunguka nchi nzima.
Watu hawakuamini kama angeweza kumaliza ziara hiyo. Lakini kwa kujitoa kwa kipekee alikokuwa nako, aliweza kumaliza ziara na kutoa burudani ambayo inakumbukwa miaka na miaka.
Alikufa kama ilivyotegemewa, lakini aliacha alama kubwa. Usikubali tatizo lolote lile unalopitia likuangushe na kukukatisha tamaa. Bali tumia kila tukio kuwa imara zaidi ya ulivyokuwa awali.
Kuchukua hatua; rafiki yangu mpendwa hata kama utakufa kesho kwa hakika, ishi kishujaa leo, ishi kwa ukamilifu leo na utaacha alama itakayodumu milele.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.