Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini chukua mfano wa mtoto mdogo anayejifunza kutembea. Atapiga hatua ya kwanza na kuanguka, lakini atasimama na kuendelea. Atajaribu tena na kuendelea.
Kwa kila anapojaribu na kuanguka, anainuka na kuendelea, hakati tamaa na kuona hawezi, atapambana mpaka aweze kutembea.
Ni kwa sababu mtoto huyo hajali maoni au ukosoaji wa wengine, anachotaka ni kutembea na anang’ang’ana mpaka aweze kutembea.
Lakini mtoto huyo huyo akiwa mtu mzima akijaribu kitu na kushindwa kisha wengine wakamwambia hawezi, anakubaliana nao na kukata tamaa.
Akiwa mtoto hakukata tamaa kwa sababu hakujali wengine wanamchukuliaje. Akiwa mkubwa anakata tamaa kwa sababu anajali sana wengine wanamchukuliaje.
Rafiki yangu kama unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako, acha kabisa kujali wengine wanakuchukuliaje. Wewe pambana mpaka upate kile unachotaka bila kujali unapitia nini.
Kuchukua hatua rafiki lengo lako siyo kuwaridhisha au kuwafurahisha wengine, bali kufikia ndoto zako. Usimsikilize yeyote anayekukosea au kukukatisha tamaa kwenye kufanyia kazi ndoto zako, zipambanie.
Akupendaye sana,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.