Imani muhimu unayopaswa kujijengea.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini imani ya kwanza na muhimu kabisa unayopaswa kujijengea ni kuamini kwamba wewe ndiye unayeyatengeneza maisha yako.

Kwamba uko hapo ulipo sasa kwa sababu ndivyo ulivyojitengeneza . Na kama unataka kuwa tofauti na ulivyo sasa, lazima ujitengeneze upya.

Kitu kimoja zaidi rafiki yangu ni kuwa matajiri huwa wanaamini wao ndiyo wamejitengeneza wenyewe na hivyo kuchukua wajibu wa maisha yao. Lakini masikini wanaamini maisha waliyonayo yametengenezwa na wengine na hakuna wanachoweza kufanya kuyabadili.

Masikini hujiona ni watu wa kuonewa na kuna njia tatu wanazotumia kuonesha hilo.

Njia ya kwanza ni kulalamika masikini hulalamikia kila kitu kwamba ndiyo kimewafikisha walipo. Hulalamikia uchumi, serikali, mazingira, wazazi, na chochote kile wanachoona ndiyo sababu ya umaskini wao.

Njia ya pili ni kuhalalisha, masikini kwa kuwa hawana fedha, utawasikia wakisema fedha siyo muhimu sana. Na hilo linawafanya wazidi kuwa masikini, kwa sababu unapoona kitu siyo muhimu, kinakukimbia.

Njia ya tatu ni kulalamika, masikini wana kila sababu na malalamiko kwa nini wao ni masikini.

Huwalalamikia wengine na hali mbalimbali kuwa chanzo cha wao kubaki kwenye umaskini. Kwa kulalamika, wanajivua wajibu wa maisha yao na kuwapa wale wanaowalalamikia, hivyo kuzidi kubaki kwenye umasikini.

Ili kuwa tajiri, amini kwamba wewe ndiye unayeyatengeneza maisha yako na hivyo chukua wajibu wa kuyatengeneza vyema.

Kuchukua hatua; rafiki yangu tunapaswa kufuta kabisa lawama, kuhalalisha na malalamiko kwenye maisha yetu. Tunapojikuta tunataka kufanya hayo matatu, tunapaswa kujikamata na kuacha mara moja.

Jiambie kuwa maisha yako ni wajibu na wewe ndiye unayetengeneza maisha yako, hivyo yatengeneze utakavyo wewe.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *