Rafiki yangu mpendwa mwandishi James W.Murphy kwenye kitabu chake cha ‘ who says you can’t sell ice to Eskimos.’ Kwenye sura ya mwisho, Murphy anamalizia kwa kutuambia kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha ni kuingiza kipato. Anasisitiza kuwa hakuna kingine muhimu kuliko hicho. Usipoingiza kipato, huwezi kupata chakula. Usipoingiza kipato huwezi kupata nyumba, huwezi kuhudumia… Continue reading Kitu muhimu kuliko vyote kwenye maisha.
Month: May 2023
Hatua 4 za kuchukua Ili kuepuka tamaa isikupoteze.
Rafiki yangu mpendwa unaweza kujiambia ukifika kwenye utajiri wa juu hutasumbuka kupata zaidi. Lakini unajidanganya, kadiri unavyopata fedha zaidi, ndiyo fursa za kupata fedha zaidi zinavyokuja kwako. Ili kuepuka tamaa isikuingie na ukapoteza kila unachotengeneza, unapaswa kuzingatia hatua haya manne. Kwanza; ujiwekee lengo lako la kifedha mapema na kisha jisukume kulifikia. Ukishafikia lengo hilo usihangaike… Continue reading Hatua 4 za kuchukua Ili kuepuka tamaa isikupoteze.
Hatua 3 za mabadiliko.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini watu wa kale walikuwa na imani kwamba madini ya risasi yanaweza kugeuzwa kuwa madini ya dhahabu kupitia mchakato ulioitwa Alchemy. Zoezi la kubadili risasi kuwa dhahabu kutokuwezekana, ilitumika sana kwenye mabadiliko ya watu. Ili mtu aweze kufanya mapinduzi makubwa kwenye maisha yake na kuzaliwa upya, alipaswa kupitia… Continue reading Hatua 3 za mabadiliko.
Nyenzo 5 za kubadili mtazamo.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini vile ulivyo ni matokeo ya mtazamo ambao unao. Matokeo unayoyapata yanatokana na mtazamo wako. Huioni dunia na mambo kama yalivyo, bali unaona kama ulivyo wewe. Hivyo ili kuona vitu kwa namna ambayo itachangia wewe ufanikiwe, unapaswa kubadili mtazamo ulionao. Kuna nyenzo tano muhimu za kufanyia kazi ili… Continue reading Nyenzo 5 za kubadili mtazamo.
Kundi 2 ya watu unayopaswa kuwaepuka.
Rafiki yangu mpendwa pamoja na vikwazo na changamoto ambazo unakutana nazo kwenye safari ya mafanikio, ipo pia changamoto kubwa ya watu wanaotuzuia tusifanikiwe. Kundi la kwanza ni wale wanazoweka wazi kabisa kuwa wanatupinga na kufanya lolote lile hili tu kutuzuia tusifanikiwe. Hawa wanatukatisha tamaa, kutuhujumu au kujaribu kutuzuia tusichukue hatua. Watu hawa ni rahisi kuwaona… Continue reading Kundi 2 ya watu unayopaswa kuwaepuka.
Namna ya kujijengea ujasiri mkubwa.
Rafiki yangu mpendwa kutoka kwenye kitabu cha ‘the everyday manifesto,’ Robin anatushirikisha hadithi ya Niki Lauda, mshiriki wa mbio za magari ambaye alipata ajali mbaya kwenye mashindano na kuungua kichwa na uso. Alipelekwa hospitali akiwa taabani na kila mtu alijua hawezi kupona. Lakini siku 40 baadaye alirudi kwenye mbio za magari, kabla hata hajapona vizuri.… Continue reading Namna ya kujijengea ujasiri mkubwa.
Njia 4 za kubadili mtazamo kuhusu fedha na utajiri.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini fedha na utajiri ni kitu ambacho kimekuwa kinawachanganya wengi. Kila mtu anataka kupata fedha na utajiri na kuweka kila juhudi ili kupata. Lakini ni wachache pekee wanofanikiwa kupata fedha na utajiri. Kinachowatofautisha wanaopata na wanaokosa siyo juhudi wanazoweka, bali mtazamo wanaokuwa nao. Kuna mtazamo ya aina nne… Continue reading Njia 4 za kubadili mtazamo kuhusu fedha na utajiri.
Njia ya kuboresha mawasiliano.
Rafiki yangu mpendwa kwa chochote kile unachofanya, unahitaji kuwashawishi watu wakubaliane na wewe. Watu hao waone na kukubali maono makubwa uliyonayo na wawe tayari kuambatana na wewe katika kufikia maono hayo. Hilo linakufanya wewe kuwa kiongozi na kiongozi bora ni yule anayefanya watu wachague kumfuata na siyo kuwalazimisha. Njia pekee ya kuwafanya watu wachague kukufuata… Continue reading Njia ya kuboresha mawasiliano.
Umuhimu wa kusikiliza kwa umakini.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini tunapaswa kuwa msikilizaji makini. Tunahitajika kusikiliza kwa makini sana pale mtu mwingine anapoongea. Tunapaswa kuweka umakini wetu kwenye kusikiliza ambacho yule anayeongea anaona tunamjali kuhusu kile anachokielezea. Kwa yeye kuona unajali anafunguka kuelezea zaidi na zaidi Atakuwa tayari kukuelezea hata mambo ambayo amekuwa anayaficha kwa sababu tu… Continue reading Umuhimu wa kusikiliza kwa umakini.
Kwa Nini Uhitaji Kufanya Kila Kitu.
Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini mtego mkubwa wa ufanisi ni pale mtu unapodhani unapaswa kufanya kila kinachokuja mbele yako, au kila ambacho watu wanataka ufanye. Pata picha unaweza kuanza na nia nzuri kwamba umalize haraka majukumu madogo madogo yaliyo mbele yako ili upate muda kwa majukumu makubwa. Lakini unapokuja kushtuka unagundua majukumu… Continue reading Kwa Nini Uhitaji Kufanya Kila Kitu.