Mambo yakufanya ili kujijengea shauku kubwa.

Rafiki yangu mpendwa kwa kuwa shauku ni muhimu kwenye kila eneo la maisha na kwa kuwa siyo kitu ambacho mtu anapewa au kunyimwa, kila mtu anaweza kujijengea shauku kubwa kwenye maisha yake.

Kwanza ni kupenda sana kile unachokifanya. Hakuna namna unaweza kuwa na shauku kubwa bila ya upendo, na siyo tu upendo wa juu, bali upendo wa kweli na wa kina, unaotoka ndani yako kweli.

Pili ni kubali sana kile unachofanya. Unapaswa kukikubali kile unachofanya kwamba ndiyo sahihi na muhimu zaidi. Usifanye kitu ukiwa na wasiwasi wowote iwapo ni muhimu au la. Kubali ni kitu na sahihi na hivyo kukifanya ni wajibu wako mkubwa.

Tatu; kuwa na kwa NINI kubwa inayokusuma kufanya kitu. Kama huna kwa nini kubwa ndani yako, sababu kubwa ya kukifanya kitu, huwezi kuwa na shauku kwenye kukifanya. Ni pale unapokuwa na sababu kubwa kabisa ndiyo unakuwa na msukumo wa kukifanya kitu bila ya kujali nini kinakuzuia.

Nne; cha manufaa ambayo wengine wanayapata kwenye kile unachofanya. Kujiangalia tu wewe mwenyewe unataka nini inaweza isikupe msukumo mkubwa sana. Lakini kuangalia kile ambacho wengine wananufaika nacho kupitia unachofanya, kunakupa msukumo mkubwa zaidi.

Tano; igiza kuwa na shauku mpaka uwe nayo. Kwa kila unachofanya, igiza kuwa na shauku kubwa, kifanye kwa moyo wako na kwa juhudi kubwa kabisa. Weka maisha yako yote kwenye kile unachofanya, kama vile ndiyo kitu cha mwisho wewe kufanya hapa duniani.

Kuigiza huko shauku kuna nguvu kubwa ya kuleta shauku kwenye uhalisia kwa sababu yetu huwa yanaathiri hisia zetu.

Kuchukua hatua; shauku ni muhimu sana kwenye maisha ya kila mmoja, wale wenye shauku ndio wanaoweza kufanya makubwa kupitia chochote wanachofanya kwenye maisha yao.

Akupendaye sana,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *