Kitu Kubwa Kinachoua Ndoto Zako.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kitu kikubwa kinachoua ndoto zako ni hofu, hofu huwa inasambaa kwa kasi ya ajabu.

Kwa kuwa zama hizi tunazoishi kila mtu ana uwezo wa kutoa habari, kupitia mitandao ya kijamii, basi hofu imezidi kuwa ugonjwa mkali. Kwa sababu mtu mmoja anaweza kuwa na hofu zake, akaanza kuzisambaza na baada ya muda mfupi kila mtu ameshaambukizwa hofu.

Ubaya wa hofu ni ngumu kutibu kwa sababu unakuwa umeimiliki, yaani hofu inaanzia ndani yako mwenyewe, hata kama umesikia tu kwa wengine.

Kuondokana na hofu hizi zinazoua ndoto za wengi, ni sawa na kuondokana na magonjwa ya virusi, yaani kinga ni bora kuliko tiba. Hivyo tujikinge na hofu za wengine, tusikubali watu watupandikizie hofu zao.

Kuchukua hatua; tunapaswa kuwa waangalifu sana kwa kukataa kutiwa hofu na wengine. Tunatakiwa tuwe na msimamo kabisa na kuamua ni nini tunafuatilia na nini hatutaki kufuatilia kwenye mtandao.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *