Kwa nini hupaswi kufurahisha kila mtu.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Winston Churchill anatushirikisha kwamba kuwa na maadui ni kitu kizuri. Inathibithisha kwamba umewahi kusimamia kitu fulani kwenye maisha yako.’

Rafiki yangu hupaswi kufurahisha kila mtu. Furahia kuwa na maoni yanayowavuruga watu. Unapaswa kubali kwamba utatengeneza maadui kadiri unavyokuwa unafanikiwa.

Lazima usimamie kitu ambacho kitawavuruga watu wengi na kuwafanya wakuchukie. Kadiri unavyochukiwa na wengi, ndivyo pia unavyokuwa unapendwa na wafuasi wako.

Wajibu wako ni kufanya kile ambacho unakipenda sana, kukifanya kwa ubora wa hali ya juu, kukifanya kwa mpango wako mwenyewe na bila kujali wengine wanakuchukuliaje.

Kitu kimoja zaidi rafiki yangu ni kwamba ambatana na wale wanaokukubali kwa vile ulivyo na unachofanya, wapuuze wale wanaokupinga na kukuchukia.

Unachohitaji kufanya Ili watu wakuchukie ni kufanikiwa sana kwa kufanya kile unachopenda kufanya. Pale unapoonyesha dalili za kufanikiwa, baadhi ya watu watakupenda na kukuunga mkono, wakati huo huo kuna wengine ambao watakuchukia na kukudharau sana.

Unachukiwa sana pale unapofanikiwa kwa sababu mafanikio yako yanawafanya wale ambao hawajafanikiwa waonekane ni wazembe. Kwa sababu hawana uthubutu wa kuchukua hatua za hatari kama wewe, furaha pekee wanayokuwa nayo kwenye maisha ni kuwachukia wale ambao wamefanikiwa.

Kuchukua hatua; rafiki hupaswi kusumbuka na watu hao, tayari maisha yao yanawaumiza vya kutosha, wapuuze na endelea kufurahia mafanikio yako.

Aliyekuwa mtawala wa Roma na Mwanafalsafa wa Ustoa, mwanafalsafa Marcus Aurelius alikuwa na maneno mazuri ya kutuambia kuhusu kutofurahisha kila mtu . Anasema kila unapoamka asubuhi jiambie kauli hii, ‘ Leo nakwenda kukutana na watu ambao ni waovu, wasio na shukrani, wenye fujo, wasaliti, wenye wivu na wasiojali. Watu hao wako hivyo kwa sababu hawajui kipi kizuri na kipi kibaya.’

Rafiki usiumie pale unapochukiwa, bali ona hizo ni dalili nzuri kwamba upo kwenye njia sahihi. Wenye chuki wana wajibu mkubwa wa kutimiza kwenye maisha yako, wanakusaidia kujenga vizuri maono yako na kukutangaza kwa wengine.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *