Mahitaji makuu 3 ya maisha.

Rafiki yangu mpendwa ili tuweze kuridhika na maisha yetu na yawe na maana kubwa kwetu, sisi binadamu tunahitaji vitu vikuu vitatu.

Kwanza; tunahitaji uhuru binafsi yaani autonomy wa kuweza kujitawala sisi wenyewe na kuchagua namna tunavyoishi maisha yetu. Pale tunapoona tunalazimishwa kuwa na maisha ya aina fulani, yanakosa maana na tunashindwa kuyafurahia.

Pili; tunahitaji ubobezi competence, uwezo wa kufanya kitu chenye manufaa makubwa kwa wengine. Tunajiona wa thamani pale wengine wanapotutegemea kwenye kitu fulani tunachofanya, pale tunapopewa sifa na hadhi kwa yale tunayofanya.

Tatu; tunahitaji kuwa sehemu ya jamii community, ambayo inatujua kutujali na kutusukuma kufanya makubwa zaidi. Ni jamii ndiyo inafanya maisha yetu yawe na maana kupitia yale tunayofanya na ushirikiano tunaokuwa nao.

Mambo hayo matatu ndiyo yanayotengeneza furaha ya ndani, furaha ambayo inadumu kwa muda mrefu.

Mambo hayo matatu ndiyo yalikuwa yakithaminiwa na kujengwa na jamii za asili. Lakini jamii ya kisasa zimehama kutoka kwenye mambo hayo ya ndani na kwenda kwenye mambo ya nje katika kutafuta furaha.

Rafiki yangu mambo ya nje yanayopewa nafasi zaidi kwenye zama hizi ni uzuri beauty, fedha money na hadhi status.

Watu wamekuwa wanakimbizana na mambo hayo wakiamini yatawapa furaha, lakini imekuwa ni ya muda mfupi tu.

Haishangazi kwa nini kwenye zama hizi, licha ya maendeleo makubwa, bado watu wengi hawana furaha na hawayathamini maisha yao.

Ni kwa sababu mahitaji ya ndani yamepuuzwa na mahitaji ya nje yamepewa nguvu.

Kuchukua hatua; rafiki yangu tunapaswa kujenga jamii zinazoweka msisitizo kwenye mahitaji ya ndani ili watu wawe huru, wawe na ubobezi na wawe sehemu ya jamii, kitu ambacho kitayapa maisha yao maana na furaha ya kudumu.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *