Kitu kinachowafanya watu wakose furaha.

Kinachowafanya watu wengi kukosa furaha kwenye maisha yao ni kuishi maisha ambayo yako chini ya uwezo wao.

Kwa mfano, mtu anajijua kwamba anaweza kuwa na maisha bora kuliko aliyonayo sasa, anaweza kufanya kazi yake kwa ubora kuliko anavyofanya sasa na pia anaweza kupata kipato kikubwa kuliko anachopata sasa lakini hakuna hatua anazochukua kufikia ule uwezo uliopo ndani yake.

Ukitaka kutengeneza maisha ya hovyo, maisha yasiyokuwa na furaha kwa kipindi chote cha maisha yako ni kupanga kuishi chini ya uwezo ulio ndani yako.

Ni bora upange kuishi kuliko uwezo wako, upange kufanya makubwa zaidi ya unavyoweza na hata ukishindwa basi utakua umeshindwa juu ya pale ulipo sasa.

Sehemu nzuri ya kuanza kuishi kulingana na uwezo wako au hata juu ya uwezo wako ni kuchukua chochote unachofikiria sasa hivi na kuzidisha mara kumi.

Kwa mfano, chukua kipato chako unachoingiza sasa, kisha kizidishe mara kumi na hilo ndiyo linapaswa kuwa lengo la kipato unalofanyia kazi.

Angalia mipango yote uliyojiwekea, zidisha mara kumi na weka juhudi kuhakikisha unafikia mara kumi hiyo.

Usiendeshe maisha ya mazoea, yasiyo na mpango, maisha ya kusubiri mambo yatokee na wewe ndiyo uone utafanya nini, utakua na maisha yasiyokuwa na furaha, maisha ya hovyo na utakuwa umechagua kupoteza maisha yako wewe mwenyewe.

Hatua ya kuchukua leo, rafiki yangu usiishi maisha yaliyo chini ya uwezo wako, amua kutumia uwezo mkubwa ulio ndani yako na utafanya makubwa kwenye maisha yako.

Rafiki yako.

Maureen Kemei.

http://www.uamshobinafsi.com/

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *