Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Robin Sharma anatushirikisha ujumbe muhimu ambao ulimjia na kusukumwa kuutoa kwa wengine.
Pata picha wakati mambo yanapoonekana kuwa magumu, unapaswa kufanya nini? Habari njema ni kuwa umepewa nafasi ya kuamini nguvu iliyo ndani yako.
Wakati wa mkanganyiko ndipo penye dirisha la kupata uelewa wa juu. Wakati unapohoji kila kitu ndiyo wakati wa ukuaji.
Wakati unapojiona mpweke ndiyo wakati umeungana na wengine wanaopitia hali kama yako.
Wakati wa dhoruba kumbuka magumu ambayo umewahi kupitia. Mawimbi makali huishia kuwa maji tulivu.
Usumbufu unaopitia wakati wa mabadiliko utageuka kuwa tulivu wa hekima mpya. Wewe ni imara zaidi ya unavyojichukulia. Una ujasiri kuliko unavyojijua. Una uwezo wa kukabiliana na chochote ambacho maisha yanakuletea.
Unapokuwa na hofu, jiulize shujaa angefanya nini? Unapokuwa na wasiwasi, jiulize kujiamini kupoje? Unapokuwa na hasira, jiulize wapi unahitaji kuwa na uelewa?
Unapokuwa na maumivu, nenda kwenye matumaini. Unapokosa kujiamini, ruhusu uongozwe na upendo.
Kila kitu kinatokea kwa manufaa yako. Hakuna kinachokuja kuondoa furaha yako. Majaribio unayopitia yatakuletea ushindi mkubwa.
Matendo yako mazuri yatazalisha mafanikio makubwa. Matokeo mazuri yako njiani kuja kwako.
Kamwe usikate tamaa.Usilinganishe safari yako na ya mtu mwingine. Unalindwa na nguvu kubwa inayoendesha ulimwengu.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
https://www.uamshobinafsi.com.