Zawadi Yenye Thamani Kubwa.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kitu kigumu zaidi kurudisha kwenye maisha ni muda uliopotea. Ukishapoteza muda, huwezi tena kuupata.

Muda ni zawadi yenye thamani kubwa, kwa sababu ni kupitia muda ndiyo tunaweza kufanya yote tunayopanga kufanya.

Lakini wapo maadui wawili ambao wamekuwa wakiiba na kupoteza muda wa wengi. Maadui hao ni uvivu na kuhairisha. Uvivu ni kutokuweka juhudi za kutosha kwenye kile unachofanya. Na kuahirisha ni kutokufanya kabisa, kuendelea kusogeza mbele yale unayopaswa kufanya.

Kama huweki juhudi za kutosha kwenye kitu unachokifanya, unaopoteza muda unaoweka kwenye kitu hicho. Na kama unahaairisha kufanya yale ambayo ni muhimu, unajua kabisa muda hausubiri wala kurudi nyuma.

Ubaya wa muda ni kwamba utaendelea kwenda, iwe unafanya yaliyo sahihi au la. Hakuna namna muda utasimama kukusubiri wewe mpaka uwe tayari. Hivyo kinachohitajika ni wewe kutumia vizuri muda ulionao, kwani ndiyo kitu pekee kinachokutofautisha na wengine.

Huwa kuna usemi kuwa muda ni pesa, lakini ni zaidi ya hapo, muda ni zaidi ya pesa, muda ni mfalme. Ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine, ukipoteza muda huwezi kupata tena mwingine. Ndiyo maana unapaswa kupangilia na kuilinda sana muda wako wa kila siku ili uweze kuutumia vizuri kufanya makubwa.

Joe Girard kwenye (13 Essential Rules Of Selling) anatushauri kuwa tunapaswa kuelewa thamani ya muda wetu, kuupangilia vizuri muda huo na kufuata kila mpango wetu bila ya kuruhusu chochote kile kituyumbishe. Kwa kuwa na mipango unayoifanyia kazi,muda unakuwa rafiki yako mzuri na siyo adui kama wengi wanavyokuwa wanachukulia.

Kwa kuupangilia muda wako vizuri hutapoteza kwenye vitu visivyokuwa na tija. Pangilia mambo yako kwa namna ambayo unakuwa na kila unachokihitaji kwa wakati husika badala ya kupoteza muda kutafuta au kusubiri kitu pale unapokuwa unakihitaji..

Siyo lazima mipango yako iwe na ukamilifu, bali unapaswa kuwa sehemu ya kuanzia kukuongoza kwenye yale unayotaka.

Kuchukua hatua; rafiki yangu sehemu ya mipango unayokuwa nayo ni kuendelea kujifunza kuhusu kile unachofanya ili kuzidi kuwa bora kwenye kukifanya.

Habari njema ni kuwa kujifunza ni kutumia vizuri muda wako ili kuweza kufanya makubwa zaidi.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *