Madhara ya kijilinganisha na wengine.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini changamoto kubwa ya watu wengi kwenye zama hizi ni kijilinganisha na wengine.

Na kujilinganisha na wengine huwa na madhara ya aina mbili.

Moja ni pale mtu anapokuwa anajiona ana uwezo mkubwa kuliko wengine, hapo husukumwa kuthibitisha uwezo wao mkubwa na hivyo kuacha kujifunza.

Upande wa pili ni pale mtu anapojilinganisha na kuona wengine wana uwezo mkubwa kuliko yeye na hivyo kujidharau na kuona hawezi.

Tafiti pia zinaonyesha kuwa wenye kupenda kujilinganisha na wengine, huwa wakishindwa kwenye maisha wanatafuta wale walioshindwa zaidi yao ili kijilinganisha nao, kitu kinachowafanya wajiskie vizuri.

Badala ya kuangalia wale waliofanikiwa kuliko wao na wajifunze kwao, wao wanataka walioshindwa zaidi, lengo siyo kujifunza, bali kujisikia vizuri, kwa sababu wanaamini uwezo wao una ukomo.

Kuchukua hatua; kinachofuata baada ya hapa rafiki, ni kuacha kujilinganisha na wengine, lakini habari njema ni kuwa una uwezo mkubwa sana ndani yako ambayo itakusaidia sana uishi kusudi lako na hivyo basi, utaacha kujilinganisha na wengine.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

uamshobinafsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *