Jinsi hatua ndogo zinavyobadili utambulisho wako.

Rafiki yangu mpendwa unajua nini kuhusu kuchukua hatua ndogo ndogo kwenye kila siku yako?

Usiwe na wasiwasi maana kuna umuhimu mkubwa wa kuchukua hatua ndogo ndogo kwenye kila siku ya maisha yako.

Habari njema ni kwamba unapoanza kuchukua hatua ndogo kwenye kupambania ndoto zako inabadili sana utambulisho wako.

Pata picha unafikiria kufanya mambo makubwa na jinsi mambo hayo yatakavyokufanikisha kwenye maisha yako.

Rafiki yangu tunaposikia hadithi za wale waliofanikiwa tunaona walivyoanza na hatua ndogo ndogo.

Sina uhakika kama itakufaa, lakini watu hao waliofanikiwa walianzia hatua ndogo ndogo kama; kusema NDIYO pale mtu alipouliza watu wa kujitolea, kuwaendea wale waliofanikiwa, kusoma kitabu au hata kuchukua kozi fulani.

Rafiki kuna aina mbili za watu duniani, wale wanaochukua hatua ndogo ndogo kila siku na kufanya bila kuacha na wale wasiochukua hatua yoyote kabisa.

Habari njema ni kwamba unapokuwa umechukua hatua moja, unajiona kama shujaa na mbobezi kwenye kitu hicho.

Kabla hujafanya maamuzi, unapaswa kufanya kitu kimoja kinachokufanya ujione ni mkarimu na utaanza kuwa na ukarimu kwenye mambo mengine.

Kitu kimoja zaidi ni kufanya kitu kimoja kinachokufanya ujione ni kiongozi na utaanza kuwa kiongozi kwenye mambo mengine.

Hatua ya kuchukua; rafiki yangu dunia inakuchukulia vile unavyojichukulia wewe mwenyewe.

Matendo yako yanaidhihirisha dunia wewe ni mtu wa aina gani.

Kinachofuata baada ya hapa ni kuchukua hatua ndogo kabisa na hiyo itakubadili kabisa.

Rafiki yako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *