Pata picha jinsi inavyokuwa rahisi sana kuwalaumu wengine, pale unapokutana na matatizo au changamoto fulani kwenye maisha yako.
Labda ni watu wamekudanganya, wamekusaliti, wamekuibia au wamekutekeleza.
Ni rahisi kuwalaumu wengine na kufarijika na kwa lawama hizo, ila sasa hazitakuwa na msaada wowote kwako.
Njia bora ya kukabiliana na hali kama hizo ni kuchukulia kila kitu ni makosa yako.
Hata kama kuna mtu kakudanganya, ni wewe umempa nafasi mpaka akakudanganya, ni wewe mwenyewe umemwamini.
Kwa chochote unachokutana nacho au kupitia, hata kama ni wengine wamefanya, bado wewe una mchango kwenye hilo.
Unapotambua mchango wako kwenye yote unayopitia, inakuwa rafisi kwako kuboresha ili usijiweke tena kwenye nafasi ya wengine kuweza kufanya mambo ya aina hiyo kwako.
Kuchukulia kila kitu ni makosa yako ni bora kuliko hata kusamehe. Maana unaposamehe bado unakuwa unaamini uliyemsamehe ndiye mwenye makosa.
Lakini unapokubali kila kitu ni makosa yako, unajiondoa kwenye hali ya mambo fulani kujirudia rudia kwako.
Kuchukua hatua; kuwasamehe na kuchukulia kila kitu ni makosa yako inakupa nguvu kubwa ya kuona kila kitu ni wajibu wako na kuweza kuchukua hatua ili kuboresha.
Rafiki yangu,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.