Rafiki yangu mpendwa, watu wengi huwa wanalalamika furaha huwa haidumu kwa sababu wanategemea kupata furaha kwenye mambo makubwa.
Hivyo wanaweka muda mrefu na juhudi kubwa kupata vitu hivyo vikubwa.
Wanapovipata wanakuwa na furaha, ila furaha hiyo huwa haidumu kwa muda mrefu.
Hilo ndiyo huwa linawaumiza watu, kwamba kwa kipindi chote walichopambania ili kukipata kitu, kinaishia kuwa cha kawaida tu kwao?
Sina uhakika kama itakufaa, lakini ili kuondokana na hali hiyo, hakikisha unapata furaha kwenye vitu vidogo vidogo.
Usisubiri mpaka upate kitu kikubwa ndiyo ukifurahie. Badala yake furahia kila hatua ndogo ndogo unayopiga. Habari njema ni kwamba kila hatua ndogo unayopiga kwenye maisha huwa haipotei.
Na hapo utakuwa na maisha ya furaha wakati wote. Usiwe na wasiwasi kwa sababu unapofanya kitu na wengine wakanufaika nacho furahia.
Chukua hatua; rafiki yangu kabla hujafanya maamuzi, tambua kwamba zipo fursa nyingi kwenye kila siku yako za kufurahia, uzitumie vizuri.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.