Mkulima mmoja alikuwa na farasi wake mmoja ambaye alimtegemea sana kwa shughuli zake.
Siku moja farasi yule akapotea na hivyo hakurudi tena. Majirani zake walikuja kumfariji, wakimpa pole na kumwambia ana bahati mbaya kupotelewa na farasi. Mkulima yule aliwasikiliza kisha akawajibu, tutaona.
Siku chache baadaye yule farasi aliyepotea alirudi, akiwa akiongozana na farasi wengine 20. Mkulima kwa kusaidiana na kijana wake waliwafinga vizuri farasi wote 21.
Majirani zake wakaja na kumpongeza, wakimwambia ana bahati nzuri kupata farasi hao wengi. Mkulima aliwajibu, tutaona.
Siku moja wakati kijana wa mkulima yule anafunga farasi wake wapya, farasi mmoja akampiga teke na kumvunja miguu yote miwili.
Wajirani wake wakaja kumpa pole, wakimwambia ana bahati mbaya kwa kijana wake kuumizwa. Mkulima aliwajibu, tutaona.
Nchi ya mkulima yule ikaingia kwenye vita. Vijana wote wenye afya walichukuliwa kwenda kwenye mapambano.
Vita ilikuwa kali na vijana wote waliuawa vitani. Lakini kijana wa mkulima alipona kwa sababu alikuwa amevunjika miguu, hakuchukuliwa kwenda vitani.
Majirani zake wakampa pongezi, kwamba ana bahati nzuri kijana wake hajafika vitani. Mkulima akawajibu tutaona.
Tunajifunza kuwa kwenye maisha tunapaswa kuchukulia mambo kama yanavyotokea kwenye maisha. Tusiwe na haraka wa kuongea sana kuhusu mambo haya maana hatujui ni lini kibaya au kizuri kitatokea.
Rafiki na mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
www.uamshobinafsi.com