Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini Derek kwenye kitabu chake cha ‘hell yeah or no,’ anatuambia huwa ana kauli mbiu moja anayoishi kwenye maisha yake, ambayo ni hii; chochote kinachokutisha ndiyo unapaswa kufanya zaidi.
Anatuambia kwa miaka 30 amekuwa akifuata kauli mbiu hiyo na imemwezesha kufanya makubwa sana.
Ikiwa chochote unachotaka, ila kinakutisha au kukupa hofu, basi ni kiashiria kwamba hicho ni kitu sahihi kwako.
Hivyo usiogope na kuacha, badala yake kikabili, na habari njema ni kwamba hapo ndipo penye ukuaji na mafanikio.
Usiwe na wasiwasi maana ukweli ni kwamba, unapokikabili kile kinachokutisha hukuiogopi tena.
Kwa sababu kinachofuata baada ya hapo unapata ujasiri mkubwa wa kuendelea kukifanya kwa viwango vya juu zaidi.
Mwanasaikolojia Abraham Maslow amewahi kunukuliwa alisema : Maisha ni mchakato endelevu wa kuchagua kati ya usalama ( kwa kuhofia na kujilinda) na hatari ( kwa kupiga hatua na kukua ). Chagua zaidi ukuaji kuliko hofu.”
Chukua hatua; rafiki yangu hivyo ndivyo unapaswa kuyaishi maisha yako, chochote kinachokutisha au kukupa hofu, ndiyo unapaswa kukifanya zaidi.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.