Rafiki yangu mpendwa kwenye kila kitu, kuna somo kubwa unaloweza kujifunza linaloendana na wewe au kile unachofanya.
Tatizo ni kuwa watu wengi hawajifunzi kwa sababu wanakuwa na ubaguzi. Wanataka mifano inayoendana na kile tu wanachofanya wao.
Unaweza kupata somo kubwa kutoka kwenye mfano wowote. Kwa mfano kitabu kinachohusu mapishi kinaweza kukufundisha mambo mengi kuhusu biashara.
Huku kitabu cha biashara kinaweza kukufundisha mambo mengi kuhusu malezi.
Usiwe na ubaguzi wa wapi unaweza kujifunza nini. Bali kwenye kila kitu, jiulize ni somo gani naondoka nalo hapa linaloendana na kile ninachofanya?
Kuchukua hatua; rafiki kwa kujifunza kwenye kila kitu, na kujiuliza ni somo gani unaondokana nalo hapa utaweza kuona masomo yalivyo mengi na yenye manufaa.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.
www.uamshobinafsi.com.