Hatua 2 Muhimu Ya Kuchukua Katika Kufanya Maamuzi Ya Kifedha.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini katika kufanya maamuzi yetu ya kifedha kwa kuzingatia bahati na hatari, tunapaswa kuchukua hatua mbili muhimu.

Moja tunapaswa kuwa makini na wale tunaowasifia na kutaka kuwa kama wao na wale tunaowadharau na kuepuka kuwa kama wao.

Tambua kwamba siyo mafanikio yote yanatokana na juhudi na siyo wote walioshindwa ni wazembe. Fikiria hii kabla hujamhukumu yeyote, hata wewe mwenyewe.

Mbili acha kuangalia hadithi ya mtu mmoja mmoja na angalia mwelekeo mpana. Unapojifunza kupitia hadithi ya mtu mmoja, huuoni ukweli, kwa sababu kuna bahati na hatari ambazo kwa nje hazionekani kwa urahisi.

Badala yake jifunze kupitia wengi ambao wamefanya kitu na kufanikiwa. Ni vigumu watu wengi wakapata bahati ya aina moja, hivyo japo kila mtu atakuwa na bahati yake, kuna vitu ambavyo wote watakuwa navyo. Ukijifunza hivyo na kuvitumia, itakusaidia zaidi kuliko kuangalia mtu mmoja.

Kuchukua hatua; badala ya kumwangalia mmoja aliyefanikiwa sana na kujifunza kwake, angalia watu wengi waliofanikiwa na kile ambacho wanacho kwa pamoja na jifunze hicho.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *