Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini changamoto kubwa kwenye hofu ni pale tunaposhindwa kuielewa kwa undani. Unapoiona hofu kwa nje inakuwa inatisha sana.
Rafiki yangu usipoichambua hofu kwa undani, hutaweza kupiga hatua, maana utaiona ni kikwazo kikubwa.
Hakuna kitu chochote kinachotokea kwenye maisha chenye maana isipokuwa ile maana ambayo tunavipa vitu.
Hivyo inapokuja kwenye hofu pia, namna tunavyoitafsiri kunaweza kuwa kikwazo au kichocheo kwetu.
Pale unapozipata dalili za hofu unaweza kuona ni mwisho na kuiacha.
Habari njema ni kwamba hupaswi kutafsiri hivyo. Wewe chukulia ni kiashiria kwamba unakaribia kufanya kilicho sahihi.
Chukua hatua; rafiki yangu mpendwa usiwe na wasiwasi maana pale unapoziona dalili za hofu kwako, jiambie wazi kwamba unakwenda kufanya kilicho sahihi na hakikisha unakifanya kweli.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.