Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kwenye maisha hakuna kushindwa, bali kuna kushinda na kujifunza.
Habari njema ni kwamba pale unapopata unachotaka unakuwa umeshinda. Lakini pale unapokosa unachotaka unakuwa umejifunza njia isiyo sahihi ya kupata kile unachotaka.
Hivyo unachopaswa kufanya ni kujifunza njia iliyo sahihi ya kupata. Unapojifunza kupitia unayokosa, unajua ni njia zipi zisizo sahihi ili usizirudie.
Kushindwa tu ni pale unapokuwa umekata tamaa au unaporudia makosa yale yale. Lakini unapokuwa tayari kujifunza na kuboresha zaidi, hakuna kushindwa badala yake kuna kujifunza.
Kukosa kile unachotaka haimaanishi kwamba huwezi kukipata, bali inamaanisha hujajua njia sahihi ya kukipata. Hivyo wajibu wako ni kujifunza njia iliyo sahihi na kuitumia.
Wewe mwenyewe ni shahidi, magumu mengi uliyopitia kwenye maisha yako na kuona kama umeshindwa, yamekuwa na mchango mkubwa kwako kupiga hatua.
Chukua hatua; rafiki yangu hakuna unachopitia kisiwe na manufaa kwako utakuwa tayari kujifunza na kuchukua hatua sahihi.
Hatua ya kuchukua;
Kwanza; orodhesha mambo yote mabaya unayohofia yanaweza kutokea. Jiulize yapi mabaya kabisa yanayoweza kutokea.
Pili; Angalia uwezekano wa kila baya ulilowahi kutokea. Ni kwa kiasi gani linaweza kutokea.
Tatu; Jiulize hatua unazoweza kuchukua pale lile baya kabisa linapotokea. Angalia kipi unaweza kufanya ili kuendelea.
Nne; Angalia manufaa makubwa unayoweza kupata kwa kuendelea kufanya.
Tano; Usikilize mwili wako ili ujue kama unachosikia ni hofu au machale.
Sita; Itumie hofu kama mwongozo kwako, kile unachohofia zaidi lakini hakitoki kwenye fikra zako, ndiyo unapaswa kukifanya.
Tano; Kumbuka magumu yote umewahi kupitia na ona mazuri uliyojifunza kupitia hayo.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.