Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kitu pekee kinachodhihirisha thamani ni kuchukua hatua ya kufanya kuliko kuongea (yaani matendo na siyo maneno). Unaweza kusema utakavyo, lakini watu wataamini zaidi kile unachofanya. Maneno ni rahisi, kila mtu anaweza kusema atakavyo. Lakini matendo ni magumu na hayo ndiyo yanayothihirisha kweli mtu anasimamia wapi. Utajiskiaje kama… Continue reading Kitu pekee kinachodhihirisha thamani yetu.
Month: July 2023
Madhara ya kijilinganisha na wengine.
Sina uhakika kama itakufaa, lakini changamoto kubwa ya watu wengi kwenye zama hizi ni kijilinganisha na wengine. Na kujilinganisha na wengine huwa na madhara ya aina mbili. Moja ni pale mtu anapokuwa anajiona ana uwezo mkubwa kuliko wengine, hapo husukumwa kuthibitisha uwezo wao mkubwa na hivyo kuacha kujifunza. Upande wa pili ni pale mtu anapojilinganisha… Continue reading Madhara ya kijilinganisha na wengine.
Imani za kujijengea ili usijiwekee ukomo.
Tambua kwamba huwezi kupata muda, bali unapaswa kutenga muda. Kama kitu ni muhimu, unatenga muda wa kukifanya . Hapa unahitaji kuweka vipaumbele vyako sawa. Tambua ukweli huu kwamba hulazimiki kufanya chochote kile. Kila unachofanya na muda wako, umechagua mwenyewe. Hakuna aliyekushikilia bastola na kukuambia usipofanya hivi nakuua. Umechagua mwenyewe hivyo mamlaka ni yako, unaweza kuchagua… Continue reading Imani za kujijengea ili usijiwekee ukomo.
Namna ya kudhibiti fikra zako.
Rafiki yangu mpendwa watu wengi hudhani hawawezi kudhibiti fikra zao. Lakini hilo siyo kweli, kudhibiti akili na fikra ni kitu kinachowezekana kabisa. Na kwa kuwa akili zetu ndiyo zinatupa kila kitu kwenye maisha yetu, udhibiti wake ni hatua muhimu ambayo kila mtu anapaswa kuifanyia kazi. Kudhibiti akili na fikra ni kitu ambacho kimekuwa kinafundishwa tangu… Continue reading Namna ya kudhibiti fikra zako.