Uongo unaokuzuiausianze.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini licha ya watu wengi kujua wanachotaka, wengi wamekuwa hawaanzi kukifanyia kazi kwa sababu wanakubali uongo ambao wamekuwa wanajiambia kwa muda mrefu.

Uongo huo ni kwamba bado hawajawa tayari. Ukweli unayopaswa kujua ni kwamba inapokuja kwenye kufanya chochote kikubwa na muhimu, hakuna wakati utajiona uko tayari.

Hofu ya kuanza huwa inajificha kwenye utayari, ili uanze lazima uvuke hofu hiyo na uwe tayari kuanza hata kama bado hujawa tayari.

Ukiyaangalia maisha yako, hatua zote ambazo umeweza kupiga, ulianza kabla hujawa tayari. Ulisukumwa kwa namna ambayo hukuwa na njia nyingine bali kuanza.

Na ulipoanza, fursa nyingi zikafunguka mbele yako na ukaweza kufanya makubwa. Usikubali uongo kwamba hujawa tayari uwe kikwazo kwako kuanza. Anza kabla hujawa tayari na utaweza kufanya makubwa.

Maendeleo yoyote kwa mtu, jamii na hata dunia kwa ujumla, huwa yanatokana na ujasiri wa mtu mmoja ambaye alikuwa tayari kuanza kabla hajawa tayari.

Kwa mtu kuanza kabla hajawa tayari kuna faida kuu mbili.

Faida ya kwanza ni kujenga ujasiri. Ujasiri ni matokeo ya vitendo na siyo maneno tu. Unapoanza kufanya kabla hata hujawa tayari, unapata ujasiri wa kuendelea kufanya.

Faida ya pili ni mwendo. Kanuni ya mwendo inasema kilicho kwenye mwendo huendelea na mwendo na kilichosimama huendelea kusimama.

Chukua hatua; kabla hujafanya maamuzi rafiki yangu tumeona umuhimu wa kuanza kabla hujawa tayari, tunapaswa kuanza kukifanya, na itakuwa rahisi kuendelea kukifanya, kuliko kungoja kuwa tayari ndio tuanze.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *