Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kuamini kwamba kila kitu kinawezekana hakumaanishi kila wakati utapata kile unachotaka.
Utakutana na watu wengi watakaokupinga na kukukatalia, watakaokuambia huwezi na haiwezekani.
Ikiwa kweli unakadiria kupata unachotaka, basi lazima ukatae kukataliwa.
Watu wanapokukatalia usikubaliane nao, wewe kataa na amini kile unachotaka kinawezekana na kuwa ta tayari kukipambania.
Hutapata ushindi mara zote, lakini njia pekee ya kujua nini hasa unachoweza kufanya ni kujaribu makubwa ambayo hujawahi kufanya.
Jenga tabia ya kuhoji kila sheria na kila ukomo ambao umeweka. Jiulize kama ni kweli au ni mazoea tu ambayo watu wanayo.
Kabla hujafanya maamuzi, unapaswa ujaribu mwenyewe kile unachoambiwa hakiwezekani badala ya kuamini tu unachoambiwa.
Na habari njema ni kwamba ni kupitia kufanya ndiyo utajifunza mengi juu ya uwezo wako, utaweza kufanya yanayowashangaza wengi.
Chukua hatua; rafiki yangu yote unayofikiria kuyafanya yatawezekana tu kama utaanza na imani kwamba kila kitu kinawezekana na kukataa kukataliwa.
Mwandishi wako,
Maureen Kemei.
kemeimaureen7@gmail.com.