Njia 5 za kukabili ukosoaji.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini pale mtu anapotoa ukosoaji wa kukukatisha tamaa, usikubaliane naye kama ndiyo ukweli. Muone kama mtu anayeleta uchafu ndani kwako.

Njia ya kwanza ni kwenye kila ukosoaji, angalia kipi ni kweli na unachoweza kutumia kuboresha kile unachofanya. Tumia hicho na puuza vingine vyote. Hapo jiulize maswali kipi ni kweli kwenye hii? Kipi naweza kutumia kuboresha na kukuza zaidi ninachofanya? Kwa kujibu maswali hayo, utaona kama kuna mazuri ya kutumia.

Angalia chanzo cha ukosoaji, mwangalie yule anayekukosoa na jiulize kama ni mtu unayemheshimu na anayejua unachofanya. Watu wanaoelewa kile unachofanya huwa hawatoi ukosoaji wa kukatisha tamaa. Ukosoaji wao huwa ni wa kujenga zaidi. Hivyo unapojua yule anayekukosoa, unajua kama upokee au upuuze.

Waonee huruma wakosoaji wanaokukatisha tamaa. Wengi wao ni watu wasio na ndoto kubwa na wasioamini makubwa yanawezekana.

Ndiyo maana wana muda mwingi mpaka wa kuwakatisha tamaa wengine. Baada ya kuumizwa na watu hao, waonee huruma, waonee huruma jinsi ambavyo hawana makubwa ya kufanya kwenye maisha yao mpaka wanakatisha wengine tamaa, ni maisha magumu sana hayo.

Cheka . Kwa ukosoaji wa wengi ambao wanakukatisha tamaa, ishia tu kucheka, hasa pale wanapokuambia mambo unayojua siyo kweli. Usibishane nao wala kutaka kuwaelewesha, wewe cheka tu.

Usimjibu mtu yeyote ukiwa na hasira, hisia kali au umelewa. Katika nyakati hizo unakuwa hufikiri vizuri, hivyo jizuie kujibu.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *