Nguvu Kuu Ya Kukataa Kukataliwa.

Rafiki yangu mpendwa sina uhakika kama itakufaa lakini kama unataka uwe na nguvu kubwa ya kuweza kukataa kila unachokataliwa.

Kama unataka uweze kuvuka kila aina ya ukatishaji tamaa na ukosoaji.

Unapaswa kuunganisha ndoto yako kubwa na kitu ambacho ni kikubwa kuliko wewe.

Unapoweka ndoto kwa ajili yako tu, ni rahisi kukata tamaa pale unapokutana na magumu.

lakini ndoto yako inapohusisha watu wengine, unapata nguvu ya kukipambania zaidi kwa sababu unajua ikishindwa siyo wewe tu unayeathirika, bali na wengine pia.

Kuwa na kusudi kubwa la maisha yako, kusudi linalokupa wajibu mkubwa na wajibu huo unakusumbua uendelee kupambana hata pale mambo yanapokuwa magumu.

Kipimo cha mafanikio ya kweli kwenye maisha yetu siyo kile ambacho tumeweza kupata, bali jinsi ambavyo tumegusa maisha ya wengine kupitia kile tunachokifanya.

Chukua hatua ; kwa kuangalia nini wengine wananufaika kupitia unachokifanya, unapaswa ulipe hilo kipaumbele, usiangalie tu ni nini unapata, bali pia angalia ni nini unatoa kwa wengine.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *