Je, Unajua Upo Hata Duniani Kwa Kusudi?

Rafiki yangu mpendwa kuna umuhimu wa wewe kujua kwamba upo hapa duniani kwa kusudi maalum.

Nadhani bado hujaweza kujua lakini haupo hapa duniani kwa ajali au bahati mbaya. Bali upo hapa duniani kwa kusudi maalum.

Habari njema ni kuwa kuna kitu wewe unaweza kufanya ambacho hakuna mwingine amewahi kufanya au atakuja kufanya. Maisha yako ni tukio la mara moja tu duniani, tukio ambalo halitakuja kujirudia tena.

Jua kusudi la uwepo wako hapa duniani na uliishi hilo, ndiyo njia pakee ya kuweza kufikia ndoto kubwa ulizonazo.

Una uwezo, vipaji, mtazamo na zawadi za kipeke, vitu ambavyo haviwezi kupatikana kwa wengine kama vinavyopatikana kwako. Vitumie hivyo kwenye kile unachofanya.

Umezaliwa na nguvu za kipekee kabisa za kuweza kuleta mabadiliko kwenye maisha yako na ya wengine pia.

Rafiki yangu usipoteze nguvu hizo kwa kuhangaika na yasiyo na tija, bali zitumie vizuri ili uweze kuleta mabadiliko ya kweli na yenye tija.

Chukua hatua; rafiki unajua unataka na unaweza kufanya makubwa zaidi ndiyo maana unasoma makala hayo. Amini zaidi kwenye hilo na chukua hatua kufanya makubwa.

Mwandishi,

Maureen Kemei.

kemeimaureen7@gmail.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *